19 Julai 2025 - 01:21
Baraza Kuu la Fat'wa la Syria: Kusaliti na kuomba msaada kwa adui wa Kizayuni ni haramu

"Adui wa Kizayuni ni adui wa wazi na ambaye uadui wake umethibitika, na kuomba msaada kwake ni miongoni mwa mambo yaliyo haramu kwa yakini."

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Baraza Kuu la Fat'wa la Syria, katika tamko lake rasmi, likisisitiza misingi ya wazi ya Sheria za Kiislamu, limetangaza kuwa aina yoyote ya usaliti na kushirikiana na utawala wa Kizayuni (Israel) ni haramu. 

Tamko hilo lilisema: "Adui wa Kizayuni ni adui wa wazi na ambaye uadui wake umethibitika, na kuomba msaada kwake ni miongoni mwa mambo yaliyo haramu kwa yakini."

Taasisi hiyo ya juu kabisa ya kidini nchini Syria iliongeza: 

"Tunasisitiza juu ya uharamu wa kuua Watoto na Wanawake, na uharamu wa kuwadhulumu raia na wasiojiweza au kuwafukuza kutoka makwao, bila kujali dhehebu lao."

Tamko hilo lilihitimisha kwa kusema: "Ni wajibu wa Serikali kuwalinda Wananchi wake wote bila ubaguzi, kuhakikisha usalama, kuzuia fitina, kuwakabili wavamizi na kuwasaidia wanyonge na waliodhuriwa."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha